




Jengo la NMB lililozinduliwa na rais Jakaya Kikwete, jana.
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi jengo jipya na la kisasa
kabisa ambalo ni makao makuu mapya ya NMB lenye ghorofa saba huku likiwa
na uwezo wa kubeba wafanyakazi zaidi ya 800. Mbali na uzinduzi wa jengo
hilo, Raisi Kikwete pia alizindua tawi jipya la benki lililo ndani ya
jengo jipya la NMB.
Uzinduzi wa jengo la makao makuu ya NMB ni mwendelezo wa maadhimisho ya
Miaka 10 ya NMB ambayo yameadhimishwa kwa mafanikio makubwa. Baadhi ya
mafanikio ya benki hiyo ni pamoja na kukuza mtaji wake mpaka kuwa benki
kubwa na bora kuliko zote nchini huku ikiwekeza vya kutosha katika
tekinolijia ya mawasiliano inayowezesha benki kumudu kutoa huduma bora
na karibu zaidi ya wateja wake.
NMB wakati inabinafsishwa mwaka 2005, ilikuwa na matawi chini ya 100,
huku ikiwa haina ATM hata moja na wateja si zaidi ya 600,000, hii leo
inapoadhimisha miaka 10 tangu kubinafsishwa, imefikisha matawi 173 na
ATM zaidi ya 600 huku ikifikisha wateja hai zaidi ya milioni mbili na
huduma zake zikienea mpaka vijijini.
Raisi kikwete aliipongeza NMB na kusema kuwa serikali inajivunia benki
hiyo huku akiahidi kuwa serikali inaitunza benki kama mboni ya jicho na
haina mpango wa kuuza hisa zake. Serikali ina hisa asilimia 32.
No comments:
Post a Comment