Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais wa tiketi ya CCM
Dkt.John Pombe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya
aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake
wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba
la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo
jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mke wa Marehemu Bi
Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya
jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
No comments:
Post a Comment