Ndege hiyo ikitokea Paris, Ufaransa kwenda Cairo Misri ilipotea ikiwa na abiria 66 kati yao wafanyakazi 10 wa ndege hiyo. Imeripotiwa kuwa ndege hiyo imeanguka katika bahari ya Mediterrania kitu ambacho maofisa wa Misri wamedai ni mapema mno kuthibitisha.
Ndege hiyo iliyokuwa ikiruka umbali wa futi 37,000 kutoka ardhini, iliruka toka uwanja wa ndege wa Charles De Gaulle, Paris na ilipotea kutoka kwenye mifumo ya mawasiliano kilometer 16 baada ya kuingia anga la Misri. |
No comments:
Post a Comment